Jumamosi , 24th Jul , 2021

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango leo ameongoza familia na wana Lupaso kwa ujumla katika shughuli ya kuhitimisha msiba wa aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa, katika ibada iliyofanyika kwenye kijiji cha Lupaso.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na kulia ni Hayati Benjamin Mkapa

Ibada hiyo imefanyika leo Julai 24, 2021, ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu alipofariki dunia Hayati Mkapa Julai 24, 2020, katika moja ya hospitali za mkoa wa Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.

"Tunakiri kwamba Mwenyezi Mungu alimjaalia kiongozi wetu huyu karama zote saba za roho mtakatifu yaani hekima, akili, shauri, nguvu, elimu, ibada na uchaji wa Mungu, mimi sina shaka kabisa kuwa Hayati Mkapa aliijua na kuisali vyema sala ya Musa kama ilivyoandikwa katika ZABURI 90:12," amesema Dkt Mpango.