Jumamosi , 30th Apr , 2022

Mwili wa Rais wa Tatu wa Kenya Hayati Emilio Mwai Kibaki unatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake Othaya Kaunti ya Nyeri nchini Kenya.

Hayati Emilio Mwai Kibaki

Msafara wa mazishi ya Hayati Rais Mstaafu wa Kenya Emilio Mwai Kibaki umeondoka asubuhi ya leo Jijini Nairobi kwa usafiri wa magari kuelekea Kaunti ya Nyeri Nchini Kenya.

Mwili wa Hayati Mwai Kibaki unatarajiwa kupitishwa katika Kaunti za Kiambu, Murang'a, Kirinyaga na baadae kufika Nyeri ili kuwapa  fursa wakazi wa maeneo hayo kumuaga kiongozi wao.

Siku ya jana maelfu ya raia wa Kenya waliungana na viongozi mbalimbali wa Kenya na kutoka mataifa ya Afrika kwenye mazishi ya kitaifa  kumwaga Mwai Kibaki, ambapo Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango alikuwa miongoni mwa viongozi walioshikiki katika hafla hiyo.

Hayati Mwai Kibaki, alifariki dunia Ijumaa  ya Aprili 22, 2022 akiwa na umri wa miaka 90.