Jumamosi , 12th Jan , 2019

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndg, Humphrey Polepole amesema kitendo cha Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad kuliita Bunge ni dhaifu ni kukikosea heshima chombo hicho kilichopewa mamlaka kamili.

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad.

Polepole ameyasema hayo ikiwa zimesalia siku chache kufika Januari 21, tarehe ambayo Mkaguzi huyo ametakiwa na Spika wa Bunge kwenda kuhojiwa na Kamati ya Maadili.

Polepole amesema kwamba watu wanapaswa kusoma Katiba ili kujua hata  tabia mbaya inaweza kumuondoa katika nafasi yake.

"Mimi nataka watu wasome tu Katiba,. Tabia mbaya inaweza kufanya Mdhibiti na Mkaguzi wa Serikali anaweza kuondolewa kwenye nafasi yake. Sijasema ana tabia mbaya hapana! Nimesema kwamba tuheshimu Katiba.Na tusipuuza Mambo, na tusizushe mambo ambayo hayapo. Si kitu kizuri" Polepole.

Polepole amesema yeye amekuwa shuhuda wa vitu vya serikali vikifanyiwa kazi bungeni, na pia kutokana na kazi zao wanapaswa kukumbushwa, kutiwa moyo na si kuwatamka kuwa ni wadhaifu "Siyo kauli nzuri ya kiuongozi.