Jumapili , 10th Apr , 2016

Hospitali ya Ngarenaro Mkoani Arusha,inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na kukosekana kwa miundombinu ya maji katika chumba cha upasuaji ambapo hospitali hiyo ambayo inahudumia zaidi ya Wakazi 74000.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda,

Akizungumzia changamoto hizo Daktari Mfawidhi wa Hospitali hiyo Josephat Kivuyo, katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Kivuyo amesema kuwa hospitali hiyo inahitaji upanuzi na ukarabati ili kuweza kuboresha huduma za afya ambazo zinahitajika na wananchi wengi.

Daktari huyo Mfawidhi amesema kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa magari ya wagonjwa maarufu kama Ambulance kwani gari lililopo ni la zamani na haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama inavyotarajiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda, amewataka wananchi na wadau mbalimbali kuunganisha nguvu katika kuboresha huduma kwa kufanya ukarabati ambao tayari umeshaanza ili kuboresha mazingira bora kwa wananchi na wahudumu wa afya.

Pia Amewataka Wahudumu wa Afya kuepuka kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa na kuwahudumia vizuri ili kupunguza malalamiko katika sekta ya afya ambayo inahudumia watanzania wengi.

Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro unaendelea na tayari hivyo nguvu ya serikali n wadau wa maendeleo inahitajika katika kuhakikisha kuwa vituo hivi vinakuwa katika mazingira rafiki ya utoaji huduma za afya.