Alhamisi , 20th Oct , 2016

Rais wa mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) Sadiki Kabab ameeleza wasiwasi wake juu ya hatua ya Burundi kujitoa kwenye chombo hicho.

idiki Kabab

Wasiwasi huo unafuatia hatua ya tarehe 12 mwezi huu ya bunge la Burundi la kupiga kura kuunga mkono mipango ya nchi hiyo kujitoa ICC.

Rais wa baraza linalosimamia mkataba wa Roma, Sidiki Kabab amesema kujitoa kwa Burundi ni kikwazo kwenye vita dhidi ya ukwepaji wa sheria, halikadhalika harakati za kuhakikisha mkataba huo unatiwa saini na nchi zote duniani.

Katika taarifa yake, Kaba amekumbusha kuwa nchi wanachama bado zina fursa ya kuwasilisha shauku zao kwa mujibu wa mkataba wa Roma na ameikaribisha Burundi kushiriki kwenye mazungumzo ya kusaka suluhu badala ya kujitoa.

Wakati huo huo ICC imemkuta na hatia Makamu wa Rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba kwa makosa yanayohusu uzuiaji wa haki wakati wa utoaji wa ushahidi kwenye kesi dhidi yake na washtakiwa wenzake watano zilizowasilishwa mbele ya mahakama hiyo.

Hukumu dhidi yao itatangazwa baadaye.