Jumatatu , 9th Jun , 2014

Zaidi ya asilimia 50 ya vifo vya akina mama wajawazito nchini Tanzania vinatokana na ukosefu wa damu katika vituo vya afya vya umma hali inayochangiwa kwa kiasi kikubwa na kutokuwepo kwa muamko wa wananchi kujitolea damu kwa hiari.

Afisa masoko wa mpango wa taifa wa damu salama Bw. Rajab Mwenda (kulia) akiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar-es-Salaam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid wakati akizungumzia maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu duniani yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 14 ya mwezi wa sita ambapo kitaifa mwaka huu yatafanyika mkoani Kigoma na mgeni ramsi anatarajiwa kuwa Mke wa Rais wa Tanzania, Mama Salma Kikwete.

Aidha Dk. Seif Rashid ameoneshwa kukera na tabia ya baadhi ya wauguzi kuwauzia damu wagonjwa wakati wakifahamu kwamba ni kinyume na utaratibu na amewataka wananchi wanaofanyiwa vitendo hivyo kutoa taarifa mara moja ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.