.jpeg?itok=tkxxxitu×tamp=1559400953)
Naibu Meya Kumbilamoto ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam alipofika eneo la City Mall, kwa ajili ya kutoa mchango wake kwa watoto wa kike waliopo shuleni kupitia kampeni ya Namthamini.
"Jambo mlilobuni EATV na EARadio ni jambo zuri sana ni la kuungwa mkono, kama Manispaa tunalibeba" amesema Kumbilamoto.
"Kama Halmashauri ya Ilala tutajitahidi kadri ya uwezo wetu, ili na sisi katika baadhi ya shule za Ilala tuweze kuzigawa hata bure, japo kwa sasa serikali imesema inaangalia utaratibu wa kuanza kuzigawa bure taulo za kike." amesema Kumbilamoto.
Kampeni ya Namthamini inayoondeshwa na EATV na EARadio kwa mwaka wa tatu sasa imeshawafikia wasichana zaidi ya 3000 na mwaka huu inalenga kuwasaidia wanafunzi wa kike zaidi ya 5000.