Alhamisi , 10th Dec , 2015

Shirika la wanawake katika sheria na maendeleo nchini Tanzania(WiLDAF) imeiomba jamii kushiriki kikamilifu katika kutoa ushirikiano kwa waelimishaji wanaojitokeza kuelimisha juu ya ukatili wa kijinsia.

Akiongea na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt. Judith Odunga amesema kuwa katika kuadhimisha siku kumi na sita za kupinga ukatili zinazoanza kesho WiLDAF imeendelea kuwataka wadau wote kushiriki kikamilifu kufahamu hali ya ukatili nchini.

Aidha Dkt. Odunga amewataka waandishi wa habari kufahamu kuwa wao ni muhimili mkubwa wa kuelimisha juu ya ukatili na kuzitumia kalamu zao kuifikia jamii.