Alhamisi , 3rd Dec , 2020

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,Simon Sirro amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi, ambapo aliyekuwa RPC wa Tabora Barnabas Mwakalukwa amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma na aliyekuwa RPC Morogoro Wilbroad Mutafungwa amekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Tanzania.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,Simon Sirro

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa hii leo ambapo IGP Sirro amesema kuwa kwa sasa hali iko shwari na bado wanaendelea na oparesheni mbalimbali ikiwemo dawa za kulevya na matuko ya unyang'anyi

Amesema hayo yamewezekana kutokana na ushirikiano uliopo kati ya vyombo vya usalama pamoja na wananchi wanaochukia uhalifu na wadau mbalimbali.

Aidha IGP Sirro ametoa wito kwa watanzania wote wenye mawazo chanya kwa nchi yao kushirikiana na vyombo vya usalama katika kubaini na kuzuia uhalifu.