
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Kamanda Mambosasa amesema hawajamkamata Mchungaji Kakobe na wala hawamtafuti kwani hajafanya kosa, na iwapo itatokea lolote umma utajulishwa.
"Hatujamkamata na hatuna 'issue' naye, hizo taarifa za kumtafuta ni habari za mitandaoni, hajafanya kosa, iwapo itatokea akakamatwa mtajulishwa", amesema Kamanda Mambosasa.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa Mchungaji huyo anatafutwa na jeshi la polisi kutokana na kauli yake aliyoitoa kuhusu Rais Magufuli.