Jumamosi , 17th Nov , 2018

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu ameagiza kulindwa kwa mipaka ya nchi, ili kuhakikisha nchi inaepukana na matukio ya kiujangili na kiugaidi ambayo yamekuwa yakizikumba baadhi ya nchi jirani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizindua jeshi maalum la maeneo ya uhifadhi (USU) ambalo litakuwa likilinda maeneo mbalimbali ya hifadhi ya utalii.

Ugaidi ni changamoto nyingine kama taifa liliwahi kupata changamoto hii japo sio moja kwa moja na haikuathiri sekta ya utalii lakini taswira yetu ilitiwa doa, ni vyema kujiweka tayari kuhakikisha maeneo yetu ya uhifadhi hayatumiki kama maficho ya waovu wa ugaidi.” alisema.

Aidha Mama Samia amesema mbali na suala hilo Tanzania imekuwa ikikumbwa na matatizo mbalimbali ya Ujangili na kupelekea kuanzishwa kwa kampeni mbalimbali za kutokomeza kwa zoezi hilo.

Kulikuwa na ukubwa wa changamoto ya ujangili, na wanyama aina ya Tembo na Faru waliathirika sana kwa kuwa  wahusika walikuwa wanatumia silaha za kivita, na tumegundua silaha nyingi zinatoka nje.” aliongeza.