Jumatano , 7th Oct , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Kenya kwa kuhutubia bunge la taifa bunge la Seneti na magavana huku akisisitiza ushirikiano wa usalama na kibiashara baina ya nchi hizo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia bunge la Kenya

Rais Kikwete amesema kuwa Serikali ya nchi hizo mbili imewekeana misimamo ya ulinzi ikiwemo kuwashughulikia wahalifu wanafanya makosa nchini Tanzania na kukimbilia nchi jirani kupita Kenya.

Aidha Dkt. Kikwete amesema kuwa viongozi wa nchi hizo waendeleze ushirikiano wao karibu kama hata baada ya yeye kumaliza muda wake wa uongozi ikiwemo kuwashughulikia wahali wanaotishia usalama wa nchi za Afrika Mashariki.

Dkt. Kikwete alilieleza bunge hilo kuwa ana uhakika mgombea urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli atashinda hivyo ana imani kubwa ataendeleza ushirikiano uliopo sasa na kuukuza zaidi.