Jumla ya watu 64,000 wametibiwa Saratani

Jumatatu , 2nd Dec , 2019

Jumla ya wagonjwa 64,000 wa Saratani wamehudumiwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, katika kipindi cha miaka 4.

Mtu akichomwa sindao

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt Julius David Mwaiselage, wakati akitoa ripoti ya mafanikio ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

"Kwa takwimu za mwaka 2018/ 2019 tulishuhudia ongezeko la wagonjwa wengi zaidi, na imefikia mara mbili zaidi mpaka sasa wamefikia 64,000, na kinachosababsha wao kuongezeka zaidi ni kutokana na huduma tunazotoa" amesema Dkt Mwaiselage.

Aidha Dkt Mwaiselage ameongeza kuwa, "Lakini pia wanaongezeka kutokana na huduma tunazowapa na wengi wao tukiwapa huduma huwa wanawaambia wenzao, na mwisho wa siku wnazidi kuongezeka zaidi".