Jumamosi , 22nd Sep , 2018

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, wa Chama cha Wananchi (CUF) Ismail Jussa amelitaja jina aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar Hamadi Masoud Hamad ambaye alijiuzulu nafasi yake kwa sababu ya ajali ya meli ya Mv Spice.

Ismail Jussa

Hatua hiyo inakuja ikiwa Taifa lipo kwenye maombolezo ya siku 4 ya kuenzi vifo vilivyotokana na ajali ya kivuko cha Mv-Nyerere ambapo mpaka sasa bado vikosi vya ulinzi na usalama vinaendelea na zoezi la uokoaji wa miili.

Kupitia mtandao wake wa kijamii Jussa ameandika "Mhe. Hamad Masoud Hamad, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutoka CUF, aliweka heshima kubwa alipokubali kuwajibika kisiasa baada ya ajali ya MV Spice Islanders na MV Skagit Zanzibar"

Septemba 10 mwaka 2011 ilikuwa ni siku ya majonzi makubwa visiwani Zanzibar baada ya meli ya Spice Islander kuzama katika eneo la Nungwi ikitokea Unguja kwenda Pemba na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000.