
Selasini ameyasema hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo ametaka kujua ni upi mkakati wa serikali katika kunusuru hali hiyo inayozidi kushika kasi kila likicha kutokana na zao hilo kukosa soko zuri pamoja na pembejeo za uhakika.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo na Ufugaji na Uvuvi Willium Ole Nasha amesema kwamba serikali inafahamu tatizo hilo na tayari imeanza kuchukua hatua za makusudi ili kurejesha zao la kahawa katika ubora wake kama zamani.
''Serikali inafahamu suala hili na tayari tumeunda mfuko maalum wa Kahawa ambao utashuhulikia kero zote na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.''- Amesema Naibu Waziri Willium Ole Nasha.