Ijumaa , 4th Feb , 2022

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa, ameipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kazi yake hasa ukamilikaji na kuanza kutumiaka kwa daraja la Tanzanite na kuziomba kamati za Bunge za mwezi Machi kufanya ziara na kupiga picha.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 4, 2022, Bungeni Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Ujenzi.

"Niipongeze serikali ya Rais Samia kwa kazi kubwa inayofanya kwenye miundombinu ya barabara, Februari Mosi daraja la Tanzanite limeanza kutiumika pale Dar es Salaam, na kamati za Machi zifanye ziara zipate kupiga picha pale" amesema Mbunge Silaa