Jumamosi , 7th Mei , 2016

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kuzingatia usafi wa mazingira ili waweze kuepukana na magonjwa ya mlipuko ambayo yangeweza kuthibitiwa kwa kufanya usafi.

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kuzingatia usafi wa mazingira ili waweze kuepukana na magonjwa ya mlipuko ambayo yangeweza kuthibitiwa kwa kufanya usafi.

Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Kawe Muta Rwakatare wakati wa Kampeni ya usafi wa mazingira inayoendelea kushika kasi katika maeneo mbali mbali nchini ambapo wakazi wa Kawe hii leo wameendesha usafi wa mazingira katika mitaa yote ya Kata hiyo.

Kampeni hiyo kwa Kata ya Kawe imefanywa kwa ushirikiano na Shirika la Msalaba Mwekundu, ambapo akiongea na East Africa Radio, Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni Dkt. Joseph Mambo amesema usafi ni muhimu katika kukabiliana na tishio la magonjwa ya mlipuko ambayo chanzo chake ni kuzagaa kwa uchafu katika makazi ya watu.