Balozi Paul Rupia
Akizungumza na East Africa TV &Radio digital hii leo, Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini.
Aidha Balozi Rupia, amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na katika Umoja wa Mataifa.
Mbali na wadhifa wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Rupia amekuwa ofisa katika Wizara ya Mambo ya Nje kuanzia mwaka 1963, pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Dar es Salaam.

