Kauli ya Polepole baada ya msemo wa TID kutumiwa

Jumatano , 5th Aug , 2020

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Hamphrey Polepole, amempa pole msanii TID baada ya yeye kulalamika kwamba msemo wake wa 'Ni yeye' kutumiwa na chama kingine ili hali alikuwa ameuandaa kwa ajili ya Rais Magufuli.

Msanii TID, na kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole.

Polepole ameitoa kauli hiyo hii leo Agosti 5, 2020, na kusema kuwa CHADEMA ni watu wa dhuluma hivyo atahakikisha wanachukuliwa hatua stahiki, kwa kuhujumu Wimbo wa Taifa pamoja na msemo wa TID.

"Nampa pole TID kwa sababu hawa majamaa wametudhulumu wimbo wa Taifa na kwakweli sisi kama Watanzania tutawachukulia hatua, TID anapambana na 'Ni yeye' ilikuwa ni ya Rais Magufuli, hawa jamaa si wameichomeka kule hawajamshirikisha wala hawajamuomba" amesema Polepole.