Jumatatu , 18th Nov , 2019

Afisa wa Jeshi nchini Kenya Peter Mwaura, amedaiwa kuwauwa kwa kuwanyonga watoto wake wawili pamoja na mkewe na kuwazika katika kaburi la pamoja eneo la Nanyuki, nchini Kenya.

Afisa wa Jeshi nchini Kenya Peter Mwaura,akiwa mikononi mwa Polisi

Maafisa wa uchunguzi wanaochunguza tukio hilo, wamesema miili ya Mama na wanawe wawili, waliotoweka wiki tatu zilizopita eneo la Nanyuki, Kaunti ya Laikipia baada ya kumtembelea Peter Mwaura, ambaye ni Afisa wa Jeshi wa kikosi cha Wanahewa cha Laikipia Airbase.

Kwa mujibu wa Afisa anayefuatilia upelelezi wa kesi hiyo Muinde Mwau, mshtakiwa Peter Mwaura atafikishwa mahakamani hii leo Novemba 18, 2019, huku upasuaji wa miili hiyo ukitarajiwa kufanyika hivi karibuni, kwa ajili ya uchuguzi wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa za mwanzo Joyce Wambua, alimtembelea aliyekuwa mumewe Peter Mwaura ambaye ni Afisa wa Jeshi, kutoka Nairobi hadi Nanyuki, lakini siku iliyofuata Wambua na mwenzake hawakuonekana, na simu yake ikipatikana kwenye gari la abiria ikidaiwa kuwa ilikuwa njama ya kupoteza ushahidi wa mauaji hayo.

Inadaiwa kuwa Afisa huyo alichukua hatua hiyo baada ya kuagizwa na Mahakama kulipa kitita cha shilingi Elfu 75000, kila mwezi kama ada ya utunzaji watoto, hii ni baada ya kuachana na mkewe pesa ambazo alizilipa kwa miezi mitatu tu kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama.

                   Mke na watoto wa wawili wa Afisa wa Jeshi ambao wanadaiwa kunyongwa