Jumanne , 6th Sep , 2016

Kampuni ya Denmark imesafirisha kutoka Kenya shehena ya kwanza ya kahawa iliyokwishaongezewa thamani, hatua ambayo inaongeza mapato ya wakulima, mara tatu zaidi.

Mkulima wa Kahawa

Kampuni hiyo ya Africa Coffee Roasters (ACR), iliyoanzishwa na msambazaji mkubwa wa bidhaa hiyo Denmark imezalisha Kenya kilo 300 za kahawa iliyokwisha tengenezwa.

Hatua hiyo inafungua milango mipya ya kuuzwa kwa kahawa iliyotenegezwa nchini Kenya kwa ubora wa hali ya juu kuuza kimataifa, ambayo awali ilikuwa ikisafirishwa kabla ya kusagwa.