Jumanne , 8th Feb , 2022

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni leo Februari 8, 2022, inatarajia kusikiliza maombi ya kesi namba 1 ya mwaka 2022, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, iliyofunguliwa na Saed Kubenea.

Katika kesi hiyo bwana Saed Kubenea anaomba kuweza kumshtaki Paul Makonda na inatajwa leo kwa mara ya kwanza mbele ya hakimu Aron Ryamuya.

Hata hivyo mjibu maombi namba 3 katika kesi hiyo ambaye ni Paul Makonda, hajaonekana mahakamani.