
Mwandishi wa Habari Saed Kubenea.
Ombi hilo linatarajiwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Augustine Mwarija. Wengine ni Jaji Dk Fauz Twaib na Jaji Aloysius Mujuluzi.
Kubenea aliwasilisha ombi hilo mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya mwanasheria mkuu wa Serikali kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala akiomba bunge hilo lisimamishwe hadi mahakama itakapotoa tafsiri sahihi ya bunge hilo kuhusu mamlaka iliyonayo na kama ni sahihi kwenda kinyume na Rasimu.
Kubenea leo alitarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuongelea ombi hilo akitaka bunge lisimame mpaka hapo ufafanuzi wa mamlaka ya bunge hilo utakapo pata tafsiri ya mahakama juu ya Mamlaka ya bunge hilo kujadili mambo ambayo hayako katika Rasimu.