Jumamosi , 6th Mei , 2023

Kesi kupinga ushindi Bola Tinubu kama rais mteule wa Nigeria itaanza kusikilizwa Jumatatu wiki ijayo ambapo majaji kutoka mahakama ya rufaa ndio watakaosikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo iliwasilishwa kupinga ushindi wa rais mteule Bola Tinubu katika uchaguzi mkuu wa mwezi Februari.
Tinubu, kutoka chama tawala cha All Progressives Congress, aliwashinda wapinzani wake akiwemo Atiku Abubakar wa chama cha the People's Democratic na Peter Obi wa chama cha Labour.

Walioshindwa wamedai kuwepo udanganyifu katika hesabu ya kura. #EastAfricaRadio,