Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu imeahirishwa leo Oktoba 24 hadi Novemba 3, 2025.
Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa mfululizo tangu Oktoba 6, imeahirishwa baada ya upande wa Jamhuri kuomba kuahirisha shauri hilo ili kupisha uchaguzi mkuu ambao upo kwa mujibu wa Katiba.
Awali, mshitakiwa Tundu Lissu, aliiomba Mahakama kutoahiriahwa kwa kesi hiyo na kama Mahakama itakubali ombi la upande wa Jamhuri basi yeye apewe dhamana kwa mujibu wa kifungu Cha 302(3).
Baada ya kusikiliza ombi la pande zote mbili,Jopo la majaji likiongozwa na Dustan Nduguru limekuja na maamzi ya kuahirisha kesi hiyo huku wakisema ombi la Mshitakiwa kuomba dhamana haliwezekani kwani kesi inayomkabili (Uhaini), haina dhamana.

