Jumatano , 14th Apr , 2021

Watu watatu, Joseph Mseth, James Mwita na Chausiku Nyangambe wote wakazi wa Ronsoti kata ya Nyamisangura, Tarime mkoani Mara wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kusafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi kilo 53.15.

Bango la Mahakama ya Wilaya ya Tarime

Watuhumiwa hao walikutwa na madawa ya Kulevya aina ya Mirungi yenye uzito wa kilo 53.15, mnamo 11-03-2021, katika eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo Mwanza wakijiandaa kusafirisha madawa hayo ya kulevya.

Washitakiwa hao wameshitakiwa kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya koso linaloangukia   Makosa ya Uhujumu Uchumi.

Kesi hiyo imeaharishwa ambapo itatajwa tena April 27-04-mwaka huu, kwa sababu Mahakama ya wilaya ya Tarime  haina mamlaka ya kusilikiza kesi hiyo mpaka kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka na watuhumiwa hao wamerudishwa mahabusu.

Wakati huo huo Kesi ya mauaji ya kijana Wankuru Nyamhanga mkazi wa Buriba Wilayani Tarime Mkoani Mara, inayomkabili Mfanyabiashara Lucas Sotel  wa Wilayani Tarime  imehaarishwa tena baada ya kufikishwa Mahakamani kwa mara ya saba.

Mfanyabiashara huyo anayefahamika kwa jina la Lucas Sotel anatuhumiwa kwa  kosa la mauaji ya kijana Wankuru Nyamuhanga, ambayo yalitendeka Agosti  09 mwaka 2014 katika kijiji cha Buriba Wilayani Tarime.

Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Bukombe Bukuru, ameiambia Mahakama kuwa Jalada la kesi hiyo lipo katika Ofisi za Mashitaka Taifa.