Jumamosi , 1st Feb , 2020

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima amehojiwa kwa takribani kwa saa 2 na dakika 55 katika ofisi za TAKUKURU - Dodoma, kuhusiana na tuhumu za viongozi wa wizara hiyo kuingia makubaliano kwa kusaini mkataba wa kununua vifaa vya zimamoto.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima na aibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni

Naibu Katibu Mkuu huyo amefika kwenye hizo asubuhi ya leo Jumamosi Januari 01, 2020 ambapo anaungana na viongozi wengine waliwahi kuhojiwa na kwenye sakata hilo.

Wakati huohuo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amefika ofisi hizo kwa ajili ya kuhojiwa majira ya saa 6 : 15 Mchana.

Hivi karibuni kwenye sakata hili aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola alifika ofisini hapo kwa ajili ya kuhojiwa kwenye sakata hili.

anuari 23, 2020 Wakati wa uzinduzi wa nyumba za Askari Magereza Ukonga jijini Dar es salaam, Rais Magufuli aliagiza kuchunguzwa kwa sakata la kusainiwa kwa Mkataba wa zaidi ya Trilioni moja na kubainisha kuwa ulikuwa hauna nia njema kwa Watanzania.