Jumapili , 8th Sep , 2019

Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla, ametangaza kujiondoa kwenye uanachama wa Chama Cha Mabaharia na kueleza tangu mwanzo kulikuwa na kusudio la kumvua uanachama.

Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla

Usemi wa baharia kwa sasa umekuwa ukitumika na watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, ukimaanisha wanaume ambao wakisaidiana mara kwa mara, hasa kwenye masuala mbalimbali ikiwemo familia.

Kigwangalla amesema kuwa, "nimeshuhudia vitendo vya mabaharia, wengi wanakiangusha chama na kwa kuwa kumekuwa na tishio la kunifuta uanachama nimeamua rasmi kuukataa''.

"Nikiwa na akili zangu timamu na bila kushurutishwa au kushawishiwa na mtu, nimejivua uanachama wa ubaharia, rasmi kuanzia muda huu" ameandika Kigwangalla kwenye Twitter.

Kwa mujibu wa Kamusi Sanifu neno Baharia maana yake ni mtu anayefanya kazi kwenye chombo cha usafiri majini, hasa baharini kama vile boti, mashua, jahazi au meli. "Mwanamaji" hutumiwa mara nyingi kwa kutaja mabaharia wa kijeshi.