Jumamosi , 25th Mei , 2019

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, amewashukuru wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/19.

''Bajeti yetu imepita salama. Kwa kishindo. Pande zote mbili zimekubaliana. Tumepewa sifa kede kede! Imani kubwa tuliyoipata kutoka kwa wenzetu ni deni la kuongeza bidii zaidi ya kazi'', amesema. 

Aidha wakati akitaja bajeti yake, Kigwangalla aliwataja baadhi ya watu ambao wizara yake inafanya nao kazi kama mabalozi wa utalii wa Tanzania, akiwataja nahodha wa taifa Stars Mbwana Samatta na msanii Alikiba.

Kigwangalla amesisitiza kuwa watu hao pamoja na wengine kama Flaviana Matata wamekuwa wazalendo kwa kuitangaza Tanzania kila wanapofanya kazi zao nje ya mipaka ya Tanzania.

Hata hivyo waziri huyo amelihakikishia bunge kuwa wizara yake itaendelea kulinda maliasili zote za nchi hii na kuhakikisha hazisafirishwi kwenda nje hata kama ni Chawa au Kunguni watalindwa.