
Jovin Godlove
Aidha ndugu hao wamesema kuwa Aprili 27 mwaka huu kuna watu walifika nyumbani wakimuulizia Jovin huku wakilalamika kwamba wakimshika watajua wao ni akina nani kwani kijana huyo ana mahusiano na mtoto wao.
Kwa upande mwingine wakazi wa kijiji hicho wanatoa rai kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuendeleza juhudi za kupambana na vitendo vya kkatili ili kuzuia taharuki kwenye jamii.
Aidha juhudi za kuwasiliana na uongozi wa jeshi mkoani humo hazikufanikiwa baada ya kumtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi bila mafaniko.