Jumatatu , 19th Sep , 2022

Mtoto wa miaka tisa anayesoma darasa la 4 katika moja ya shule za msingi zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amebakwa mara kadhaa na kijana anayefahamika kwa jina moja la Seif (27), huku akimrubuni kuiba pesa kwa mama yake na kumpelekea yeye.

Mtoto aliyebakwa

Tukio hilolimeleta maumivu makubwa Kwa mama yake ambaye  anazungumza kwa shida kutokana na uchungu alionao baada ya mtoto wake kutendewa kitendo hicho cha ukatili.

Mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho cha ukatili ameeleza hali halisi ilivyokuwa mpaka kufikia hatua ya kufanyiwa ukatili mara kwa mara na kutokusema kwa mzazi.

Kwa upande wake daktari wa hospital teule ya rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt. Boniphas Lyimo, amethibitisha kumpokea mtoto huyo na vipimo vimebaini ameingiliwa kimwili.