
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo hii leo Desemba 7, 2020, wakati akizungumza na wakuu wa mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Maafisa Biashara wa mikoa, mawakala wa saruji walioko mikoani na wakurugenzi wa viwanda vya saruji, kikao ambacho kimefanyika kwa njia ya video.
"Mfano saruji inazalishwa Tanga au Dar es Salaam, halafu Morogoro inauzwa kwa Tsh 28,000, sasa Kigoma itauzwaje lazima kuwe na bei kikomo", amesema waziri Mkuu.
Aidha Waziri Mkuu meongeza kuwa suala hilo halihitaji kuundiwa bodi kwa sasa, kwani vyombo vya kusimamia biashara vipo, wizara husika ipo, hivyo amewataka wahusika wote wahakikishe wanasimamia suala hilo kikamilifu ili kuwawezesha wananchi kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu.