
Rais John Magufuli
Rais ameyaongea hayo jana wakati alipokuwa anapokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita, walimu pamoja na watumishi wa umma, ambapo wafanyakazi zaidi ya elfu tisa wamesimamishwa kazi papo hapo kwa kosa la kufoji vyeti.
"Tanzania haijasema mpaka uwe na elimu ya 'Degree' au zaidi ndiyo utaweza kuajiriwa serikalini. Kila mtu afanye kazi kutokana na elimu yake, usilazimishe kufanya kazi zisizoendana na 'qualification' yako kwa sababu tukikugundua tutakuchukulia hatua. Ukiacha na suala la kughushi vyeti kuwa kosa, watu wanaofanya uhalifu huo ni majambazi kama jinsi walivyo majizi wengine". Alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ametumia siku hiyo kuwaonya waajiriwa wa serikali waliofoji vyeti kuondoka katika nafasi zao na kuwapisha vijana wanaozunguka mitaani na vyeti kutafuta ajira.