Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kilichojiri kwa CAG Assad baada ya kuhojiwa

Jumatatu , 21st Jan , 2019

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Prof. Musa Assad leo amehojiwa kwa zaidi ya saa tatu naKamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka, kutokana na kauli yake ya kuliambia bunge ni dhaifu wakati akihojiwa na redio moja nchini Marekani hivi karibuni.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Prof. Musa Assad akiwa kwenye Kamati ya Maadili leo asubuhi.

Saa tano kamili asubuhi akisindikizwa na maafisa wa bunge Pof. Assad ameingia bungeni kisha kujiandikisha katika kitabu cha wageni kabla ya kuingia ukumbi wa mahojiano saa 5 na dakika sita ambako alihojiwa hadi saa 8:47 mchana.

Akizungumza na wanahabari baada ya mahojiano ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka, Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka amekiri kwamba CAG amehudhuria mahojiano na kutoa ushirikiano mkubwa hivyo mapendekezo yatapelekwa kwa spika Job Ndugai.

“Ametoa ushirikiano wa kutosha na amejibu maswali yote ambayo alikuwa anaulizwa na wajumbe. Shahidi Profesa Assad ametoa ushirikiano wa kutosha. Ametusaidia kwa kila hatua tuliyofikia na kila swali aliloulizwa amejibu, tunamshukuru sana,” alisema Mwakasaka.

Kikao hicho kilihusisha karibu wajumbe wote 18 wa Kamati.

Januari 7, 2019 Spika Job Ndugai alimtaka CAG kufika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli yake ya aliyoisema akiwa nje ya nchi kwa kusema kuwa  bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni dhaifu.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi