Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kilomita 111.4 za barabara zakamilika Mkoani Mara

Jumapili , 17th Mar , 2024

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha miradi mitatu ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya  Kilomita 111.4  Mkoani Mara

.Miradi hiyo ni Ujenzi kwa kiwango cha lami Barabara ya Nyamuswa - Bunda-Bulamba(Km 56.4), Makutano juu - Sanzante (km 50)  pamoja na barabara ya Musoma - Busekela(Km 92), kipande cha kwanza cha kutoka Kusenyi - Suguti (km5).

Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mara, Mhandisi Vedastus Maribe amesema hayo tarehe 13 Machi 2024 alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya ujenzi.
“ tunaishukuru Serikali yetu chini ya Mama yetu, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa kiasi cha shilingi Bilioni 137.165 ili kutekeleza mradi wa barabara hizi tatu ambazo ujenzi wake umekwishakamilika” amesema Mha. Maribe

Amesema kufunguliwa kwa barabara hizo kumeongeza uchumi wa Mkoa kwa kurahisisha usafiri kwa watalii wanaokuja nchini kuelekea Katika mbuga ya Serengeti; pia zimechochea fursa kwa wafanyabishara wa madini kuweza kuuza madini yao katika soko la kimataifa pamoja na  kurahisha  huduma ya usafiri wa kutoka Mkoa Mara kwenda Mikoa Jirani kwa uharaka zaidi tofauti na hapo awali.

Ametaja Miradi mingine inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara ya Sanzante- Nata ( Km 40), Mogabiri-Nyamongo ( Km 25), Tarime-Mugumu-(Km 87.14) sehemu ya Tarime-Mogabiri ( Km 9.3), Nyamongo-Mugumu (Km 48.15, na barabara ya Mzunguko ya Mugimu ( km 3.6), Ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha ndege Musoma, pamoja na Ujenzi wa Mzani wa kupima magari yakiwa kwenye mwendo.

Pia, ameishukuru Serikali kwa kuwajali Wakandarasi Wazawa kwani Miradi yote ya 
Matengenezo ya barabara imefanywa na wakandarasi hao ikiwa ni juhudi za Serikali kuwajengea uwezo.
Mha. Maribe amesema  taa zaidi ya 608 za barabarani zimefungwa katika maeneo ya Musoma mjini, Bweri, Nyabange, Butiama, Kiabakari, Sabasaba, Pida, utegi, mika, Mazami, Makutano (ziroziro) pamoja na Nyanchabakenye na mwaka huu wa fedha taa nyingine zaidi ya 336 zitaendelea kufungwa kwenye maeneo ya Kusenyi, Musoma Manispaa, Nyamuswa, Komaswa, Bitaraguru, Nyamika na Olio.

Ametoa wito kwa wananchi kuwa walinzi wa Miundombinu ya barabara ikiwemo taa na alama za barabarani na kuheshimu hifadhi ya barabara kwa kutofanya shughuli zozote kwenye maeneo hayo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

HABARI ZAIDI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi