Jumanne , 2nd Sep , 2025

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesafiri kwenda China kwa treni kuhudhuria gwaride kubwa la kijeshi,

Kim Jong Un anatarajiwa kuungana na Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Urusi Vladimir Putin na viongozi wengine wa dunia katika tukio hilo la kihistoria.

Gwaride hilo la dakika 70 huenda likaonyesha silaha za hivi karibuni zaidi za China, zikiwemo mamia ya ndege, vifaru na mifumo ya kuzuia ndege zisizo na rubani - mara ya kwanza muundo mpya wa jeshi lake unaonyeshwa kikamilifu katika gwaride.

Kiongozi huyo aliyejitenga husafiri mara chache sana, huku mawasiliano yake ya hivi majuzi na viongozi wa dunia yakimhusisha Putin, ambaye amekutana naye mara mbili tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Korea Kaskazini Jumatatu ilionyesha kuunga mkono matamshi yaliyotolewa na Xi katika mkutano wa kilele unaotaka utawala mzuri wa ulimwengu, na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya Korea Kaskazini na China utakua kwa sababu ya masuala kama hayo, kulingana na Makamu wa Mambo ya nje aliyetoa maoni yake katika tovuti ya wizara ya Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini.

Makumi kwa maelfu ya wanajeshi watashiriki gwaride hilo maalum litakalofanyika uwanja wa kihistoria wa Tiananmen Square mjini Beijing, kuadhimisha miaka 80 ya Japan kujisalimisha katika Vita vya Pili vya Dunia na kumalizika kwa mzozo huo.

Viongozi wengi wa Magharibi hawatarajiwi kuhudhuria gwaride hilo, kwa sababu ya kupinga kwao uvamizi wa Urusi wa Ukraine, ambao umesababisha vikwazo dhidi ya serikali ya Putin.