Jumanne , 26th Apr , 2022

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amelihutubia jeshi la nchi hiyo na kusema kuwa , mipango ya kuendeleza shughuli za nyuklia nchini ipo na kutaka kazi hiyo iendelee.

Ametoa hotuba yake katika paredi ya jeshi hilo ambapo pia kulikua na maonesho ya makombora ya masafa marefu yaliyopigwa mafuruku ya  intercontinental ballistic missiles (ICBMs).

Mwezi jana , Korea Kaskazini ilifanya majaribio makubwa ya makombora hayo yenye uwezo ywa kutoka bara moja hadi jingine , ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2017, ambapo hali hiyo ilipelekea ukosoaji mkubwa kutoka kwenye jumuiya za kimataifa. 
 
Marekani iliweka vikwazo kwenye nchi hiyo baada tu ya jaribio hilo.  Silaha zaidi zilioneshwa katika sherehe za jeshi hilo ikiwemo meli kubwa aina ya nyambizi yenye uwezo wa kubeba silaha nzito .  

Bw. Kim amekua hatikiswi na vikwazo vyovyote dhidi ya nchi yake , na kwamba jana alisema kuwa

 ‘Tutaendelea kuchukua hatua za kuimarisha na kuendeelza mipango yetu ya kukuza uwezo wa  Nyuklia kwa nguvu zaidi , vikosi vyote vya nyuklia vijipange kwa ajili ya mazoezi muda wowote ule’’