Alhamisi , 29th Sep , 2022

Kimbunga kikubwa kuwahi kutokea kimeipiga Marekani katika jimbo la Florida na kuacha mamilioni ya watu bila huduma ya umeme na mafuriko makubwa kabisa.

 Kimbunga Ian hatimaye kimetua Marekani kikitokea Cuba huku kikiwa na upepo mkali unaofikia umbali wa kilomita  241 kwa saa.

Kimbunga hicho kimeleta uharibifu mkubwa  ikiwemo kuharibu hosptali, magari na miti mikubwa kuanguka barabarani. 

Wakazi wa Florida wameonywa kwamba saa 24 zijazo zitakua za hatari zaidi  ambapo kunatarajiwa kutokea mvua kubwa na upepo mkali utakaodumu usiku kucha .

Kimbunga Ian kinatarajiwa kuelekea Kaskazini mwa Florida katika uwanja wa ndege wa Jacksonville ambao umesitisha safari zote za ndege.