Jumamosi , 17th Sep , 2022

Maelfu ya raia wa nchini Japan wametakiwa kuondoka kwenye makazi yao kutokana na onyo la uwepo wa kimbunga hatari kinachotarajiwa kupiga maporomoko ya Kyushu  siku ya kesho

Kimbunga hicho kiitwacho Nanmadol  kinatarajiwa kuvuma kesho kikiwa na upepo mkubwa utakaovuma kwa kilomita 270 kwa saa huku mvua kubwa zikitarajiwa ndani ya saa 24 zijazo.

Tahadhari kutoka eneo la  Kyushu, zinasema kwamba kutakua na maporomoko ya udogo na mafuriko  makubwa, huku huduma za susafiri wa treni na ndege zikisitishwa. 

Kyushu ni kisiwa kilichopo kusini mwa nchi hiyo  kikiwa ni kisiwa kikubwa kati ya visiwa vinne ambavyo vinaunda Japan na kinakadiriwa kuwa na watu wanaofikia  milioni 13.