Mwili wa Nickson Myamba, ukiagwa kanisani
Mauaji hayo ya kutisha ambayo siyo ya kawaida kuwahi kutokea katika maisha ya kanisa hilo la Mtakatifu Bikira Maria Mama wa Neema, ambapo marehemu aliuawa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
Akizungumza katika misa ya mazishi ya kiongozi huyo wa kanisa aliyeuawa ndani ya duka la vitabu vya imani, Padre Jordani Mwajombe, Decanusi wa Makambako amewataka waumini kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi.




