
Liz Truss alimrithi Boris Johnson na kuwa waziri mkuu 6 Septemba 2022.
Akizungumza nje ya Downing Street, Liz anasema amemwambia Mfalme Charles kwamba anajiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative.
Kulikua na vuguvugu kubwa la kumtaka Bi Liz Truss mwenye umri wa miaka 47 kujiuzulu wadhifa aliodumu nao chini ya miezi miwili .
Liz Truss aliyekaa madarakani siku 45 tu , ataendelea kuwa waziri mkuu mpaka wiki ijayo atakapopatikana mrithi wake.
Wabunge wa chama chake walimtaka Bi Truss kuachia nafasi hiyo baada ya serikali yake kukumbwa na misukosuko ya kisiasa, kufuatia kuondolewa kwa sera zake nyingi za kiuchumi.
Bi Truss alisema chama cha Conservative kilimchagua kwa mamlaka ya kupunguza kodi na kuongeza ukuaji wa uchumi.
Amekiri kwamba hataweza kutimiza malengo ya chama chake kwa kile anachotakiwa kufanya kama inavyotakiwa.
B. Truss anakua ni kiongozi aliyekaa muda mfupi kuliko waziri mkuu yoyote kuwahi kutokea nchini Uingereza.
Ilikua ni siku ya jana tu, katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu , Bi Truss alisisitiza kuwa yeye ni "mpiganaji, sio mtu wa kukata tamaa" baada ya kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer kwamba kwa nini hajajiuzulu.
Lakini vugu vugu zaidi liliongezeka baada ya viongozi wengine waandamizi akiwemo Suella Braverman alipojiuzulu kama waziri wa mambo ya ndani na kura ya kupinga udanganyifu ilianguka, huku baadhi ya wabunge wa Tory wakituhumiwa kwa uonevu.
Liz Truss alimrithi Boris Johnson na kuwa waziri mkuu 6 Septemba na kujiuzulu siku ya leo 20 Oktoba 2022. Rekodi ya nyuma ka Waziri mkuu aliyeshikilia madaraka kwa muda mfupi zaidi ni George Canning aliyekaa siku 119 pekee, ambapo alifariki dunia akiwa kwenye utawala mwaka 1827.
Liz ni Waziri mkuu wa mwisho kabisa kuthibitishwa na marehemu Malkia Elizabeth kabla hajafariki, na utawala wake kuanza na siku 10 za maombolezo ya kitaifa.