Alhamisi , 3rd Feb , 2022

Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi, amesema kwamba uchaguzi wa kumpata Naibu Spika wa Bunge hilo utafanyika Februari 11, 2022, na kuvitaka vyama vyenye wawakilishi Bungeni kushiriki na kianze mchakato wa kumpata mgombea kutoka miongoni mwa wabunge wa chama hicho.

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 3, 2022, hii ni baada ya aliyekuwa Naibu Spika ambaye sasa ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, kuandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo mnamo Januari 31 mwaka huu.

Jina la mgombea litatakiwa kuwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi kabla ya saa 10:00 jioni siku ya alhamisi ya Februari 10, 2022.