Jumatatu , 26th Oct , 2020

Meneja msimamizi wa kituo cha mabasi ya daladala cha Makumbusho Haidery Salum amesema kwa sasa wanefanikiwa kudhibiti wimbi la vibaka ambao walikuwa wakiwaibia abiria  katika kituo hicho.

Pichani ni Kituo cha Mabasi ya Daladala cha Makumbusho.

Akiongea na EATV, leo Haidery, amesema wanefikia hatua hiyo mara baada ya kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kwa kuweka vijana walinzi ambao wanekuwa wakiwakamata vibaka na kuwafikisha kituo cha polisi cha Mabatini

“Kwa sasa changamoto ni wapiga debe lakini nayo tunaishughulikia muda si mrefu tutaimaliza” amesema Haidery

Naye mmoja wa vijana walinzi katika kituo hicho Issa Mohamedi,amesema mbinu wanazozitumia kuwakamata vibaka ni wao kama walinzi kujifanya nao ni abiria na ndipo wanawabaini vibaka kwa urahisi.