Jumanne , 11th Aug , 2020

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema kunahitajika zaidi ya magari 24 ya kubebea wagonjwa katika hospitali za serikali za mkoa wa Dar es Salaan kutokana na yaliyopo kwa sasa kutokidhi mahitaji.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Jamhuri ya watu wa Korea

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema kunahitajika zaidi ya magari 24 ya kubebea wagonjwa katika hospitali za serikali za mkoa wa Dar es Salaan kutokana na yaliyopo kwa sasa kutokidhi mahitaji.

Mganga Mkuu ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Jamhuri ya watu wa Korea kupitia Shirika lake la Maendeleo la KOICA ambavyo vitagaiwa katika hospitali tano za mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa KOICA Kyucheol Eo amesema KOICA itaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania katika nyanja mbalimbali kwa lengo kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Jamhuri ya Korea.