
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo katika ofisi zake Ilala, Jijini Dar es salaam amesema analipongeza jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuhakikisha wanapambana kupunguza misongamano barabarani.
"Athari za mafuriko zinachangiwa na mambo mengi moja wapo kubwa ni mabadiliko ya tabia nchini mara nyingine jangwani hapapitiki lakini Dar es salaam mvua hazijanyesha kiasi kikubwa lakini tayari pana mafuriko"RC Kunenge
"Kuhusu 'traffic'nawapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha jiji letu linakuwa halina misongamano ya lazima ingawaje wakati mwingine wanazidiwa na sisi tunaona"ameongeza RC Kunenge
Aidha amesema anamshukuru Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli katika tamko lake la kujenga daraja katika eneo la Jangwani ili kuepukana changamoto ya mafuriko na kufungwa kwa barabara hiyo.