Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 22, 2022, wakati akishiriki Jubilee ya miaka 25 ya utumishi wa kiaskofu wa Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge, Ngara mkoani Kagera.
"Baba Askofu umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hiyo si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine, maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie, na sio nijitukuze kwenu," amesema Rais Samia



