Jumatatu , 6th Dec , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba anajitahidi kufanya anavyoweza ili kuiweka nchi kwenye hali nzuri kwani hata siku yake ikifika akaulizwa na Mungu ni kipi alichokifanya ataeleza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 6, 2021, wakati akizindua kiwanda cha Elsewedy Electronic East Africa Limited kilichopo Kisarawe II, Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

"Unaambiwa ukiwa kiongozi una maswali ya kujibu kwa Mungu, na mimi ndiko ninapopaogopa zaidi, nafanya ninavyoweza ili nikifika huko kesho na keshokutwa nikiulizwa niseme nimefanya hiki, kwa usafi, kuliko kwamba ooh nilisema sikusikilizwa, nataka nijisafishie njia yangu," amesema Rais Samia.