
Mwanafunzi wa darasa la Saba ajifungulia chumba cha mtihani
Afisa elimu wa Mkoa huo, Majuto Njaga amesema kwamba tukio hilo lilitokea Julai 27, 2022 wakati mwanafunzi huyo akiwa katika chumba cha mtihani.
Afisa elimu huyo amesema kwamba idara ya elimu wilayani Maswa ilitoa taarifa katika ofisi yake na kueleza kwa kipindi chote cha ujauzito walimu hawakuwa wanafahamu kama mwanafunzi huyo ni mjamzito.
"Alijifungua akiwa shuleni, baada ya kujifungua ofisi ya elimu kwa kushirikiana na maafisa wa ustawi wa jamii walifika shuleni hapo na binti alimtaja aliyempa ujauzito na tayari kesi imefunguliwa," - Majuto Njaga, Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu