
Moshi kama unaoonekana pichani hapo juu ni hatari kwa afya ya binadamu.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar-es-salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau wa mafuta nchini na mamlaka ya udhibiti wa mafuta na nishati EWURA kwa lengo la kujadili athari za kutumia madini mengi ya Salfa kwenye mafuta.
Kwa mujibu wa meneja wa ufundi wa masuala ya Petroli kutoka EWURA, Bw. Gerald Maganga amesema kutokana na madhara hayo. Tanzania sasa itakuwa nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki iliyofanikiwa kupunguza Salfa kwenye mafuta ya Petroli na Dizeli.