Jumamosi , 12th Jan , 2019

Moja ya wanasiasa ambao kwa mwaka 2018 walikuwa ni watumiaji wa wakubwa mtandao wa Twitter ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambaye alionekana kutoa maoni yake kwenye masuala mbalimbali ya kitaifa lakini kwa mwaka 2019 pia ameendeleza utaratibu wake wa kutoa maoni yake juu ya masuala

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

yanayotokea nchini.

www.eatv.tv imekueletea baadhi ya maoni yake yaliyozua gumzo kaika mtandao wa Twitter juu ya masuala mbalimbali yaliyotokea nchini.

Januari 02, 2019 siku moja baada ya Rais Magufuli kutoa salamu za mwaka mpya ambapo alikemea tabia ya watumishi wa umma kuogopa kauli ya kuwa ni maagizo ni kutoka juu.

Mbunge Lema aliandika, "Rais anapaswa kufahamu kuwa "maelekezo kutoka juu" unatokana zaidi na attitude na tabia, kwani attitude ndiyo inayotoa mwelekeo wa nchi na attitude kwa wasaidizi wa Rais."

Januari 6, 2019 Mbunge huyo aliandika, "hofu ni kubwa katika jamii kwa matendo yenu, biashara zimeharibika, wawekezaji wanaondoka, taasisi hazifanyi kazi kwa uhuru, Siasa/demokrasia imekuwa ni chuki, hali ni mbaya na mbinu ya kurekebisha hamna,mlifikiri CHADEMA ndiyo kikwazo cha akili zenu na kumbe ni nyie"

Januari 6, 2019 aliandika, "kubomoa uchumi ni kazi nyepesi ,hauhitaji IGP apeleke FFU barabarani, matamko tu yanatosha, sijui kama mnaona hatari ya njaa / umasikini uliyoko mbele..."

Katika sakata la kuitwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Profes Juma Assadi Mbunge huyo aliandika, "kwa vile utawala wa sheria, katiba sio msingi tena, ni dhahiri kabisa kuwa CAG Assad anaweza akavaa pingu kama Spika alivyosema".

 

Leo Januari 12, 2019 Lema ameandika, "maamuzi ya serikali kufunga maduka ya kubadilisha fedha za kigeni Arusha, yameimarisha biashara haramu ya fedha, kama Serikali ikiendelea kuchelewa kufanya maamuzi ya maduka haya biashara hii itaimarika."